Warsha ya Kiswahili iliyojumuisha shirika la wanahabari, wahariri na waandishi kutoka 'Nation Media' Tarehe 19/03/2024

Chama Cha Kiswahili Katika Chuo Kikuu Cha Eldoret (CHAKIUOE) ni Chama ambacho kilianzishwa mwaka wa 2016 kwa madhumuni ya kuwapa wapenzi wa lugha ya Kiswahili jukwaa maridhawa la kushabikia Kiswahili, kuinua viwango vya utafiti na hata kulea vipaji vya wanafunzi katika sanaa zinazofungamana na lugha ya Kiswahili.

Tarehe 19/03/2024, Naibu Makamu Chansela Profesa Wilson Ng'etich aliwapokea Wadau kutoka shirika la Nation Media ambayo walipata nafasi ya kutagusana na wanafunzi wanaokienzi Kiswahili Chuoni. Profesa alipongeza juhudi wanazozitia wanafunzi katika kukishabikia Kiswahili huku akisisitiza kuwa mustakabali wa lugha pamoja na sera zake sharti ziweze kuimarishwa chuoni kwani Kiswahili kina umaarufu na pia kina nafasi pevu. Katika mapokeo, Afisa Muenezi na anayesimamia shughuli za kuuza sera za Chuo pamoja na kukipa umaarufu Bi. Cynthia hakukosa, alishabikia swala hili la kupigia Kiswahili Chapuo. Mkuu wa Idara ya mawasiliano, lugha na Fasihi Dkt Seraphine vile vile alijiunga na wengine katika kunadhifisha warsha hiyo. Dkt Angela Sawe ambaye alikuwa ndiye Mhadhiri wa siku alipongezwa kwa kufanya mipango bora na kuhakikisha kuwa Kiswahili kinaimarika na kupata umaarufu chuoni, amewalea waandishi wa kazi ya Fasihi, kama vile Riwaya na Hadithi Fupi, katika taarifa aliyotoa, aliahidi kutochoka na juhudi za kukipigania Kiswahili na kulea magwiji wa Lugha.

Kikosi Cha Nation Media kilipata fursa ya kuzungumzia nafasi ya Gazeti la Taifa Leo katika kukikuza Kiswahili. Jana ilikuwa siku ya kushabikia na kujivunia ukwasi wa lugha katika Chuo kikuu Cha Eldoret.

Self Service

Independently access, perform and obtain services from our enhanced automated systems

Menu